“MSD simamieni matumizi sahihi bidhaa za afya”

MTWARA: BOHARI ya Dawa (MSD) Kanda ya Mtwara imekumbushwa kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia matumizi sahihi ya bidhaa za afya ili kuleta tija kwa wananchi.

Hayo yamesemwa wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wateja na wadau wa Kanda ya MSD Mtwara mwaka 2024.

Mkutano huo umefanyika mkoani Mtwara wenye kauli mbiu  “Tuzungumze Pamoja Kutatua Changamoto za Upatikanaji wa Bidhaa za Afya”

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauteri Kanoni amesema kwa kutekeleza hayo wananchi watapata huduma bora zaidi katika vituo vya kutolea huduma za afya bila manung’uniko.

Amesema serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuongeza fedha inayotengwa kwa ajili ya bajeti ya kununulia bidhaa za afya ili kuboresha utoaji wa huduma hizo.

“Kuhakikisha mnakuwa na majadiliano yenye tija ya namna bora ya kufanya kazi kwa pamoja ili kila upande uweze kutimiza wajibu wa kuhudumia mwananchi”amesema Kanoni

Aidha amewaagiza kwenda kusimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha kufanya hivyo kutasaidia vituo viweze kulipa madeni yaliyopo MSD kwa wakati mara baada ya kupokea shehena ya bidhaa na kuepuka madeni yasiyo ya lazima.

Meneja wa MSD Kanda ya Mtwara, Tea Malay amesema wanatoa huduma katika mikoa miwili ikiwemo Lindi, Mtwara.

 

Habari Zifananazo

Back to top button