Mshahara unatoka kwenu – Makonda

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, (CCM) Paul Makonda amesema amechaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kutatua kero za wananchi sababu ndio wanampa mshahara.

Amesema mgogoro wa shamba la maua la Kiliflora utapata majibu ili wafanyakazi wanaodai fedha zao wapumue.

“Viongozi mjipange nimekuja Arusha kwa mambo matatu,utalii,kero za wananchi ikiwemo uhamasishaji wa maendeleo,”amesema

Na mabango yenu ndio yanatupa taswira ya utekelezaji wa ilani ya chama chama mapinduzi, maana mwandishi wa ilani ya chama huandika vizuri lakini utekelezaji wake unaweza kudanganywa basi nasoma mabango haya na kila anayeguswa kuhusuana na mabango ya wananchi ajiandae kutoa majibu sahihi”

Habari Zifananazo

Back to top button