Mshambuliaji Scotland afariki dunia
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Scotland, Jim Forrest amefariki dunia leo.
Forrest aliwahi kucheza Rangers ya nchini humo, amefariki akiwa na umri wa miaka 79. Pia aliwahi kucheza na Aberdeen, Preston North End na San Antonio Thunder.
“Familia ya Rangers leo imehuzunishwa na kumpoteza mshambuliaji wa zamani, Jim Forrest, akiwa na umri wa miaka 79.” Imeeleza taarifa ya Ranger kwenye mtandao wa X.