Mshambuliaji Ufaransa afariki dunia
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Ufaransa, Just Fontaine amefariki.
Fontaine anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kombe moja la Dunia, amefariki akiwa na umri wa miaka 89.
Fontaine alifunga mabao 13 katika mechi sita pekee za Ufaransa kwenye Kombe la Dunia la 1958 nchini Uswisi na timu yake kumaliza nafasi ya tatu.
Nyota huyo katika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji mabao wa muda wote wa Kombe la Dunia pamoja na Lionel Messi wa Argentina.
“Nyota wa soka ya Ufaransa, mshambuliaji bora, mchezaji maarufu wa Reims, amefariki” ilisema klabu yake ya zamani ya Stade de Reims.
Aliwahi pia kucheza Paris St-Germain,