Mshenga atumbuliwa
RAIS wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi ametumbua Meneja wa Shirika la Umeme la Zanzibar (Zesco) Mshenga Haidar Mshenga.
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said imesema kuwa utenguzi wa Mshenga umeanza leo Agosti 29, 2023
Itakumbuka Mshenga aliteuliwa kushika wadhifa huo Mei 4, mwaka huu, hivyo kudumu kwenye nafasi hiyo kwa miezi mitatu na wiki tatu.