Mshindi bingwa msimu wa pili kubeba Crown

KAMPUNI ya Startimes Media imetambulisha zawadi ya gari aina ya Toyota Crown yenye thamani ya Sh milioni 20 itakayotolewa kwa mshindi wa shindano la bingwa msimu wa pili katika fainali itakayofanyika wiki ijayo.

Shindano la bingwa msimu wa pili lilizinduliwa Julai mwaka huu na kushirikisha washiriki 24 ambao ni maarufu mitandaoni waliokaa katika jumba moja maalum kuonesha uhalisia wa maisha yao na kuoneshwa kwenye televisheni ya Tv3.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema mshindi wa jumla sio tu ataondoka na gari bali fedha taslimu ambazo itakuwa ni kama ‘surprise’ zitakazoenda kumsaidia kuendesha maisha yake.

“Tunawashukuru sana Watanzania wanaoendelea kufuatilia vipindi vyetu, msimu huu wa sikukuu tunawaambia Lipa Tukubusti, lipia vifurushi tofauti upate nyongeza na kushuhudia fainali hii kuona bingwa ni nani msimu huu,”alisema.

Kwa upande wake, Meneja mradi wa shindano hilo, Ombeni Phiri alisema washiriki wamebaki 12 walioingia fainali hivyo, wataendelea kuchuana hadi wiki ijayo mshindi mmoja ataondoka na gari hilo.

alisema washiriki hao wakiwa ndani ya jumba hilo walijifunza vitu vingi ikiwemo fursa za kutumia mitandao ya kijamii kujiinua kiuchumi na kukuza majina yao.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button