Msigwa amshukuru Rais Samia
“Nawashukuru wote mlionipigia simu na kunitumia ujumbe wa kunipongeza.
” Ameandika Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa mara baada ya Rais Samia kumteua kushika nafasi hiyo.
Msigwa amendika “Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake na kunisimamia daima. Namshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kuniteua katika jukumu hili la Katibu Mkuu.
Kwangu hili ni deni, naahidi kulilipa kwa utumishi uliotukuka,”
“Nawaomba tuendelee kuombeana kheri ili jukumu nililopewa na matarajio ya Mhe. Rais na wadau wote wa Utamaduni, Sanaa na Michezo yatimie.” Ameandika Msigwa.
Uteuzi wa Msigwa kwenye wizara hiyo umefanyika leo, ambapo nafasi ya Msemaji wa Serikali itapangiwa mtu mwingine kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu.