Msigwa ateta na Watendaji wa Wizara

DAR ES SALAAM: Katibu Mkuu Wizara ya utamaduni Sanaa na Michezo. Gerson Msigwa amewataka wakuu wa taasisi za wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia falsafa ya kufanya kazi kwa  upendo pamoja na ubunifu ili watekeleze majukumu ya taasisi hizo kwa ufasaha wa maendeleo ya nchi.

Katibu Mkuu, Gerson Msigwa ametoa kauli hiyo leo Novemba 22,2023 jijini Dar es salaam alipokutana na kuzungumza na wakurugenzi na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara akiwasisitiza waendeleee kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali.

Aidha,Amewataka viongozi hao waendeleee kujenga uwezo wa taasisi zao kwa kuimarisha vitengo vya habari na mawasiliano kwa kutangaza shughuli zao kupitia vyombo vya habari ili watanzania wajue kazi kubwa zinazofanywa na taasisi hizo

Pia,Msigwa amewasisitiza viongozi hao waendelee kuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuweka mikakati itakayosaidia taasisi hizo kutumia mazingira na fursa zilizopo kuongeza mapato yatakayosaidia taasisi hizo kukabiliana na changamoto mbalimbali huku akitoa wito kwa viongozi hao watumie vyema taaluma za watumishi wanaongoza katika eneo la ubunifu na kujali maslahi yao.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button