Msigwa ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Sanaa, Michezo
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na Michezo.
–
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhuru Yunusu imeeleza kuwa nafasi ya Msemaji wa Serikali na nafasi ya Mkurugenzi Habari Maelezo itatangazwa hapo baadaye
–
Katika taarifa hiyo pia imeeleza Rais Samia amemteua Othman Yakubu kuwa Balozi.
–
Kabla ya uteuzi huo Othman Yakubu alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na Michezo.