Msigwa: Simba waliupiga mwingi dhidi ya Al Ahly

DAR ES SALAAM: Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema Simba walipoteza mchezo wa jana dhidi ya Al Ahly lakini walikuwa bora zaidi uwanjani.

Akizungumza na Wachezaji wa Simba baada ya mtanange huo, Msigwa amesema muda mwingi Al Ahly waliteseka uwanjani kutokana na ubora wa Simba.

Ameongeza licha ya kupoteza bado Simba ina uwezo wa kwenda kupindua meza nchini Misri kwenye mchezo wa mkondo wa pili Aprili 5, 2024.

Simba ilipoteza bao 1-0 hivyo inahitaji matokeo ya ushindi yenye faida zaidi ya Al Ahly ugenini ili kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Habari Zifananazo

Back to top button