Msitumie madalali maduka ya kubadili fedha

KAGERA; Bukoba. Wafanyabiashara ambao wanaomba lesseni za kufungua maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wametakiwa wasitumie madalali.

Ushauri huo umetolewa na maofisa wa BoT waliofika mkoani Kagera na kutoa ufafanuzi juu ya kanuni mpya za mwaka 2023 zilizofanyiwa marekebesho kutoka kanuni za mwaka 2019 kuhusu kufungua maduka na matawi ya kubadilishia fedha za kigeni.

Mkuu wa kitengo cha uchunguzi BoT, Amri Mbalilaki amesema kuwa kanuni za mwaka 2023 za kumiliki duka la kubadilisha fedha za kigeni zimepunguza mtiririko wa vikwazo vingi kwa Watanzania wazawa kupata leseni za umiliki, ukilinganisha na miaka ya nyuma, hivyo hakuna sababu kutumia dalali ambaye atachukua fedha nyingi kwa mfanyabiashara bila sababu.

Amesema kuwa kwa miaka iliyopita mfanyabiashara aliyetakiwa kufungua duka la kubadilisha fedha za kigeni alipaswa kuwa na mtaji wa Sh bilioni moja na kuendelea lakini kwa sasa serikali imeondoa kikwazo icho kwani mfanyabiashara ambaye anamtaji wa Sh milioni 500 anaweza kumiliki duka la kubadilisha fedha za Kigeni.

Omary Msuya Meneja msaidizi katika Kitengo cha usimamizi wa fedha kutoka Bank Kuu akitoa elimu juu ya Manufaa ya kuwa na fedha za kigeni kwa watanzania alisema ni kuhakikisha fedha zinadhibitiwa na zinajulikana kiasi chake kuliko kuziacha zikabadilishwa kiholela katika mitaa na kutoa mwanya kwa matapeli ambao wakiziona mtaani wanatengeneza fedha za kigeni bandia na kuwasababisha hasara wafanyabiashara wasiokuwa na elimu ya utambuzi wa fedha hizo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
SandyLayman
SandyLayman
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by SandyLayman
Marry
Marry
1 month ago

●Im making over $13k a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life.(ss)last month her pay check was $12712 just working on the laptop for a few hours. This is what I do, ↓↓↓↓VISIT THIS WEBSITE↓↓↓↓
HERE☛…..☛ http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x