‘Msiwafiche watoto wenye usonji’

DAR ES SALAAM: Imani za kishirikina, kuhofia aibu pamoja na elimu duni dhidi ya watoto wenye hali ya usonji ni moja ya sababu ya baadhi ya wazazi kushindwa kuwaonesha watoto hao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji Asasi ya kijamii ya Lukiza Autism Foundation, Hilda Nkabe jijini Dar es salaam wakati alipotembelea shule ya msingi Msimbazi Mseto kitengo cha watoto wenye usonji kwa lengo la kuhamasisha jamii kutowaficha watoto hao ambapo ameiomba serikali kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya usonji.

Dk Isack Maro ameitakla jamii kutowaficha watoto hao ili washiriki pia fursa zinazopatikana katika jamii huku akitaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo kuwa ni Mtoto kushindwa kujumuika na wenzake pamoja na kuwa na tabia za kujirudia rudia.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake ana hali ya usonji amewasihi wazazi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wao wenye viashiria vya usonji huku Attu John ambaye ni mmoja wa wadau wa maendeleo akisisitiza umuhimu wa wadau kushiriki moja kwa moja katika kusaidia jamii zenye mahitaji mbalimbali

Habari Zifananazo

Back to top button