Msiwanyweshe pombe watoto- DC Mgomi

SONGWE; WAZAZI wilayani Ileje mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwanywesha pombe watoto wadogo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kufifisha juhudi za Serikali katika kupambana na utapiamlo pamoja na udumavu kwa watoto.

Agizo hilo limetolewa leo Aprili 4, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi alipokuwa katika kijiji cha Kabale kata ya Kalembo wilayani humo alipohudhuria maadhimisho ya wiki ya lishe na afya vijijini ambayo hufanyika kila baada ya robo mwaka.

“Kila mtu anataka kuona mtoto wake kesho na kesho kutwa anaitwa Dokta Joyce, kesho keshokutwa mtu anataka kuona mtoto wake anaitwa Mkuu wa Wilaya, Farida Mgomi, kesho na kesho kutwa anataka kuona mtoto wake anaitwa nani! ofisa lishe Esther Mshana,” amesema DC Mgomi.

Maadhimisho ya Wiki ya Lishe na Afya vijijini katika Wilaya ya Ileje yanalenga kutoa elimu na hamasa juu ya umuhimu wa lishe hasa kwa watoto wadogo kuanzia miaka 0-5 ikiwa ni sehemu ya lengo la Serikali kupambana na changamoto ya udumavu pamoja na utapiamlo.

Habari Zifananazo

Back to top button