‘Msiwaoze wanaosubiri matokeo la saba’

JESHi la Polisi Mkoa wa Katavi, limewaonya wazazi na walezi mkoani humo watakaobainika kuwaoza watoto wao waliohitimu darasa la saba, litawachukulia hatua.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, ACP Ali Makame, amesema hakuna mtoto ambaye atafaulu na kushindwa kujiunga na sekondari kwa vile serikali imejipanga vya kutosha kuboresha miundombinu ya vyumba vya madarasa.

Makame amesema ni jukumu la kila mzazi kumlinda na kuwatunza vijana wao waliomaliza mitihani yao ya darasa la saba, wakati huu wanaposubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha kwanza.

“Isitokee mzazi akaitumia hii kama ni fursa ya kwenda kumuozesha au kumuoza kijana wake, tukigundua hilo hatutasita kumchukulia hatua kwa kumkamata, lakini pia kumshitaki,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x