Msonde: Msiwaogope viongozi kutekeleza utendaji

MAOFISA elimu nchini wametakiwa kuwaheshimu viongozi lakini wasiwaogope ili yale yanayoelekezwa na serikali yatekelezeke.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), anayeshughulikia Elimu, Dk Charles Msonde akifunga kikao kazi cha maofisa elimu mikoa na wilaya kilichofanyika jijini Dodoma.

Amesema, maofisa hao elimu wanapaswa kusimamia miradi ya elimu kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo na kutoruhusu vikwazo vya kukwamisha utendaji kazi wao.

“Heshimu viongozi waliopo juu yenu lakini msiwaogope ili yale yanayoelekezwa na serikali yatekelezeke kwa kuwa lengo la hii miradi ni ya Lipa Kulingana na matokeo litimie.”Amesisitiza Msonde na kuongeza

“Hivyo kinachohitajika ni kuisimamia ikamilike kwa wakati kwa kuwa mahitaji ya kujenga shule za msingi na sekondari ni makubwa mno,”amesema.

Aidha, amesema vipo vikwazo wanavyopitia maofisa hao katika utekelezaji wa miradi hiyo lakini wasiache kusimamia sheria na taratibu ili ikamilike na kuanza kupokea wanafunzi ifikapo Januari 2024.

“Kuweni wajasiri simamieni sheria na taratibu zilizowekwa hakuna fedha zinazoletwa kwenye halmashauri bila mwongozo, mtu yeyote asikutoe kwenye reli simamia maelekezo bila kuangalia mtu,”amesema.

Kadhalika, ameagiza maofisa hao kufanya tathmini ya miundombinu iliyokwama ikiwamo maboma yaliyojengwa na wananchi ili kupata gharama halisi zitakazosaidia serikali kutafuta fedha za kuikamilisha.

“Fanyeni tathmini kupata gharama sahihi na ndogo ambazo serikali ikipata fedha itaweza kugharamia, kwa mfano miradi ya EP4R, na majengo yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi,” amesema.

Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu TAMISEMI, Vicent Kayombo, amesema katika kikao hicho wameangalia namna ya kuimarisha ubora wa elimu nchini na kutoka na maazimio 11 ikiwamo kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
1 month ago

Earn money in USA, high scores from trusted resources. Work at your own pace. Regular Payments. Search in different job categories. Work anywhere on your vs03 computer, laptop or mobile phone. Update your profile at any time.
.
.
Detail Here———->>> http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Julia
Donna Lentz
Donna Lentz
1 month ago

I­ g­e­t­ p­a­i­d­ o­v­e­r­ 220 D­­­­­­­­­­o­­lla­­­­rs p­e­r­ h­o­u­r­ w­o­r­k­i­n­g­ f­r­o­m­ h­o­m­e­ w­i­t­h­ 2 k­i­d­s­ a­t­ h­o­m­e­. i­ n­e­v­e­r­ t­h­o­u­g­h­t­ i­’d­ b­e­ a­b­l­e­ t­o­ d­o­ i­t­ b­u­t­ m­y­ b­e­s­t­ f­r­i­e­n­d­ e­a­r­n­s­ o­v­e­r­ 15k­ a­ m­o­n­t­h­ d­o­i­n­g­ t­h­i­s­ a­n­d­ s­h­e­ c­o­n­v­i­n­c­e­d­ m­e­ t­o­ t­r­y­. it was all true and has totally ch­a­n­g­e­d­ ­m­y­ l­i­f­e­. T­h­i­s­ ­i­s­ ­w­h­a­t­ ­I­ ­d­o­,­ ­c­h­e­c­k­ ­i­t­ ­o­u­t­ ­b­y­ ­V­i­s­i­t­i­n­g ­F­o­l­l­o­w­i­­n­­g ­W­e­b­s­­i­t­e

CO­PY HE­RE →→ http://Www.Smartwork1.com

JaylenJordin
JaylenJordin
1 month ago

★ I’m making $90 an hour working from home. ( a66q) i was greatly surprised at the same time as my neighbour advised me she changed into averaging $100 however I see the way it works now. I experience mass freedom now that I’m my non-public boss. Everybody must try this job now by just using this website..
CLICK HERE ——————->> http://www.SmartCareer1.com

Last edited 1 month ago by JaylenJordin
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x