Msuva, Kabylie waachana

KLABU ya JS Kabylie ya Algeria imetangaza kuvunja mkataba na mshambuliaji wa Tanzania, Simon Msuva kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Msuva alijiunga na klabu hiyo Agosti 2023 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Qadisiya ya Saudi Arabia.
Mwaka 2017, Msuva alijiunga na Difaa Al Jadid ya Morocco akitokea Yanga, msimu wa 2020 alisajiliwa na Wydad Casablanca ya nchini humo kwa mkataba wa miaka minne.

Akiwa na Difaa alifunga mabao 5 na kutoa pasi za mabao matatu katika mechi 28.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *