Mtaala mpya wa elimu kuibua vipaji

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa mapitio ya mitaala ambayo yataongeza masomo na kozi mbalimbali zilizojikita kutoa zaidi ujuzi utakaowawezesha wahitimu kujiajiri.

Aidha imepokea ushauri wa Mbunge wa Viti Maalum, Naghenjwa Kaboyoka ya kutumia bidhaa zinazotokana na ubunifu wa wanafunzi kuviingizia vipato vyuo na shule.

Katika Swali lake la msingi, Mbunge huyo aliitaka kufahamu endapo serikali inaona umuhimu wa kuanzisha masomo yatakayoibua vipaji vya watoto.

Akijibu Swali hilo Bungeni, Dodoma leo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema: “Serikali inatambua umuhimu wa masomo yanayoibua vipaji vya watoto kuanzia ngazi ya Elimu ya Msingi.
“Kwa kuliona hilo Wizara ilianzisha somo la Sayansi na Teknolojia kuanzia Darasa la Tatu, Stadi za kazi pamoja na Sanaa na Michezo.”

Amelieleza Bunge kuwa katika masomo hayo, mada mbalimbali zinazochochea vipaji zinafundishwa.
Akitolea mfano somo la Stadi za Kazi, Naibu Waziri amesema, wanafunzi hujifunza muziki, uigizaj, ufinyanzi na ususi

“Katika somo la Michezo na Sanaa, wanafunzi hujifunza Michezo Sahill, Michezo ya Jadi, Riadha na Mpira,” ameongeza.

Naibu Waziri amesema, kwa upande wa somo la Sayansi na Teknolojia, wanafunzi hujifunza Matumizi ya Nishati, Majaribio ya Kisayansi, Mashine na Kazi na Kuelea na Kuzama kwa vitu.

Aidha, Wizara imetoa mwongozo wa Ubainishaji na Utambuzi wa wanafunzi wenye Vipawa na Vipaji wa mwaka 2022.

Amelihakikishia Bunge kuwa Serikali kwa sasa inaendelea na mapitio ya mitaala.

Habari Zifananazo

Back to top button