Mtaka awapa angalizo ambao hawajahesabiwa

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Antony Mtaka (pichani) ametoa mwito kwa wananchi ambao hawajahesabiwa watumie siku zilizobaki kwa faida yao na nchi yao.

Mtaka alitoa kauli hiyo jana baada ya kuona kazi hiyo inavyoendelea kwenye maeneo mbalimbali.

“Niwaombe wananchi wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kushiriki kikamilifu zoezi hili, kwa yeyote ambaye hatajitokeza ajione kama ana deni la maisha kwa maana kwamba kama hujahesabiwa unaenda kutumia haki ya mwingine ambayo wewe hukuishiriki,” alisema.

Mtaka alihimiza makarani wa sensa waifanye kazi hiyo kwa umakini, weledi na uadilifu kwa kujiepusha na vitendo vya ‘Ngoswe’ wakati wanapotekeleza jukumu hilo lenye faida kubwa kwa Taifa.

Aliomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa wanapopita kutekeleza wajibu wao.

Aidha, aliviomba vyombo vya habari kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwaelimisha wananchi kujitokeza na kushiriki zoezi hilo muhimu kwa kuwa wapo baadhi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu sensa.

Habari Zifananazo

Back to top button