Mtama watakiwa kuepuka chuki za kisiasa

MBUNGE wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema jamii ijielekeze katika kufanya kazi za maendeleo badala ya chuki za kisiasa.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa jimbo hilo katika Ofisi ya Mbunge wa Mtama na kusisitiza kuwa kipindi hiki hasa kwa vijana ni cha kufanya kazi kujipatia maendeleo ya kiuchumi.

Amesema si vyema kila kukicha watu kukaa vijiweni na kujengeana chuki za vyama vya CCM na Chadema, huku viongozi wa ngazi za juu wa vyama hivyo wanazungumza wakati wananchi wa kawaida wanajengeana chuki na maneno yasiyofaa.

Pia amewataka vijana kuchangamkia fursa katika mgosi wa Nammangale utakapoanza kufanya kazi mwakani, baada ya kukamilika kulipwa fidia kwa wanainchi waliopisha mradi.

Habari Zifananazo

Back to top button