Mtambo wa kuhifadhi mbegu wazinduliwa Arusha

WIZARA ya Mifugo imezindua mtambo wa kuzalisha hewa baridi ya Nitrogen wenye zaidi ya Sh milioni 700 utakaotumika kuhifadhi mbegu za mifugo uliopo  Wilaya ya Arumeru Jijini Arusha katika kituo cha Taifa cha Uhamilishaji (NAIC)

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa, Riziki Shemdoe amesema serikali imepanga kuboresha mbegu za mifugo kwa kutumia madume bora na kwa njia ya uhimilishaji.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na mifugo inayofugwa kuwa na tija ndogo kwenye uzalishaji wa nyama na maziwa na kuongeza kuwa asilimia 97 ya ng’ombe nchini ni ng’ombe wa asili wenye uzalishaji mdogo hivyo idadi iliyobaki ni ndogo na inapaswa kuongezwa kundi la ng’ombe wanaozalisha nyama na maziwa kwa wingi ili kutosheleza mahitji ya walaji nchini na malighafi za viwanda .

Ambapo katika mwaka huu wa fedha, wizara imegawa madume bora 366 ya nyama kwa vikundi vya wafugaji katika halmashauri nane ili kuzalisha ng’ombe bora wa nyama ambapo wizara inaendelea na zoezi la uhimilishaji katika halmashauri mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kuzalisha kwa njia ya uhimilishaji na kuongeza idadi ya ng’ombe bora wa nyama na maziwa.

Kaimu Mkurugenzi kituo cha uhimilishaji NAIC, Dk Dafay Burakai amesema lengo la mtambo huo ni kuboresha uzalishaji wa mifugo kwa kutumia teknolojia ya uhimilishaji ambapo teknolojia hiyo ni rahisi kueneza kutokana na ng’ombe waliyopo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na nyama pamoja na kupunguza gharama itokanayo na kuagiza nyama na maziwa kutoka nje ya nchi sambamba na kuzuia magonjwa yanayoenezwa kupitia mfumo wa uzazi.

Kituo hicho kina jumla ya madume ya Ng’ombe 34 yaliyogawanyika katika makundi manner ambapo dume moja anauwezo wa kuzalisha dozi 100,000 kwa mwaka,na kusema kuwa kituo hicho kilikuwa na changamoto ya kuzalisha kimiminika cha hewa baridi ambapo uwepo wa mtambo huo kutasaidia uwezo kwa kuongeza na kuboresha uzalishaji wa mbegu bora .

Habari Zifananazo

Back to top button