Mtangazaji BBC afariki dunia

MTANGAZJI wa Shirika la Habari la BBC, George Alagiah amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 67, wakala wake ameeleza.

Mwanahabari huyo mzaliwa wa Sri Lanka alianza kwenye kipindi cha BBC One’s News At Six mwaka 2007, mwaka 2014 aligundulika kuwa na saratani ya utumbo mpana iliyokuwa imesambaa kwenye ini.

Baada ya matibabu ya muda mrefu Oktoba 2015 alitangaza kurejea BBC na kurudi kwenye kipindi cha BBC One’s News At Six Novemba 10 mwaka huo.

Alagiah alijiunga na BBC mwaka wa 1989 na alitumia miaka mingi kama mmoja wa waandishi wa habari wa kigeni.

Habari Zifananazo

Back to top button