Mtanzania adakwa na Dawa za Kulevya Afrika Kusini

MAMLAKA ya kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Afrika Kusini imemkamata Ahmadi Mbwana Chonde (50) ambaye ni raia wa Tanzania akiwa na kilo mbili za dawa za kulevya aina ya heroin.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA,) usiku wa kuamkia leo, imesema kuwa Chonde, mwenye hati ya kusafilia yenye namba TAE145658, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa jijini Cape town siku ya Jumanne Desemba 20, 2022.

Taarifa hiyo ya DCEA imesema kuwa Chonde, alikua kaficha dawa hizo za kulevya ndani ya sanduku lake la nguo alilokuwa akisafiri nalo kutoka Capetown kuelekea nchini India katika miji ya Kochi na Chennai kupitia Doha.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x