Mtanzania aweka rekodi Valencia Marathon

Mwanariadha Mtanzania, Gabriel Geay ameweka rekodi kwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya ‘Valencia marathon’ akitumia saa 2:03:00 kukimbia mita 10,000 katika mbio za wanaume, akizidiwa dakika mbili na mshindi Kelvin Kiptum raia wa Kenya.

Kelvin Kiptum ameshinda mbio hizo akitumia saa 2:01:53, ikiwa ni mara ya kwanza kutumia muda huo mchache katika historia. Ushindi huo unamfanya Kiptum kuweka rekodi ya dunia iliyokuwa ikishikiliwa na mkenya mwenzake, Eliud Kipchoge huku akiwa mchezaji wa kwanza wa mbio za marathon mwenye kasi zaidi kuwahi kutokea.

Gabriel Geay aliwahi kutumia saa 02:04 kumaliza mbio za Toronto Marathon na kuvunja rekodi iliyowekwa na Augustino Sulle, Oktoba 2018 kwenye mbio hizo zilizofanyika nchini Canada.

Mwanariadha mwingine raia wa Kenya, Alexander Mutiso alitumia saa 2:03:29 kwa mara ya kwanza, akishika nafasi ya tatu. Tamirat Tola raia wa Ethiopia alishika nafasi ya nne akitumia saa 2:03:40 na Ozbilen Kaan Kigen wa Kenya alishika nafasi ya tano akitumia saa 2:04:36.

Upande wa wanawake Beriso Shankule Amane, raia wa Ethiopia ameweka rekodi kwa akitumia saa 2:14:58 na kushika nafasi ya kwanza. Gidey Letesenbet alishika nafasi ya pili akitumia saa 2:16:49, wakati Chepkirui Sheila raia wa Kenya akishika nafasi ya tatu akitumia saa 2:17:29

Habari Zifananazo

Back to top button