Mtemvu ashinda uwenyekiti CCM Dar es Salaam

MBUNGE wa zamani wa Temeke Abbas Mtemvu ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kupata kura 444 na kumwangusha Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mama Kate Kamba aliyepata kura 160.

Kate Sylivia Kamba ameshindwa kutetea nafasi yake hiyo ambayo aliongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Mkoa Fatma Mwasa, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alimtaja mshindi huyo katika ukumbi wa Mawela Sinza jijini Dar es Salaam.

Mwasa amewataja wagombea wengine kuwa ni aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Temeke 2002, Baraka Konisaga kura nne na aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Kamishna wa Polisi Jamal Rwambow kura mbili.

Kwa upande wa nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wametoka wawili wawili katika wilaya zote tano. Amewataja wilaya ya Ilala kuwa ni Mashaka Nyadhi kura 371 na Ramadhani Ponela kura 360.

Wilaya ya Kigamboni ni Abubakari Abubakar kura 465 na Haran Sanga kura 330. Kwa Wilaya ya Temeke walioshinda ni Issa Mangungu kura 454 na Mariam Kambi Kura 301.

” Ubungo ni Ashura Sendondo 378 na Meshaki Mangula 332. Vile vile wilaya ya Kinondoni ni Idd Azzan na Francis Nanai,” amesema.

Pia alitajjwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni Juma Simba 437.

Akishukuru baada ya kutangazwa mshindi, Mtemvu ameahidi kuwatumikia wananchi na Taifa, usiku na mchana bila kumdhulumu mtu haki yake na hatakubali dhuluma. “Kitu nachochukia kikubwa ni rushwa hayo sutakubali wana Ccm wafanyiwe,” amesema.

Amesema sasa watajipanga kwa uchaguzi wa madiwani na Rais mwaka 2025.

Habari Zifananazo

Back to top button