BREAKING: MTENDAJI Mkuu wa Manchester United, Richard Arnold ataondoka katika nafasi hiyo mwishoni mwa mwaka huu, BBC Sports imeripoti.
–
Mhasibu huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukua nafasi ya Ed Woodward kama mtendaji mkuu wa United mnamo Februari 2022.
–
Kuondoka kwake, ambako bado hakujathibitishwa rasmi, kunakuja wakati Kampuni ya INEOS Group ya Sir Jim Ratcliffe ikijiandaa kukamilisha ununuzi wa asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo.
–
Mkataba huo unatarajiwa kupitishwa katika kipindi cha mapumziko ya kimataifa mwezi huu.
–
Home Mtendaji Mkuu Man United kuachia ngazi
Comments are closed.