WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, wamemchagua Method Mtepa, kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, baada ya kuwashinda Emmanuel Manamba na Mweji Kabudi.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika Uwanja wa Azimio, msimamizi mkuu wa Uchaguzi Wilaya ya Mpanda, Joseph Lwamba amesema Method Mtepa alipata kura 532, huku wapinzani wake kila mmoja akipata kura 150 kati ya kura 852 zilizopigwa, ambapo kura 20 ziliharibika.
Pia msimamizi huyo wa uchaguzi alimtangaza Elias Mwanisawa kuwa Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Wilaya ya Mpanda, baada ya kupata kura 81 dhidi ya mshindani wake wa karibu Gilbert Kaswiza aliyepata kura 48.
Akizungumza Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Abel Kimazi, ametoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kudumisha umoja, mshikamano na upendo na kuendeleza mema yaliyoanzishwa na uongozi wake.