KLABU ya Mtibwa Sugar imesitisha mkataba na kocha Habib Kondo kwa makubaliano ya pande zote mbili.
–
Mtibwa wametoa taarifa hiyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.
–
Taarifa hiyo inasomeka “Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili uongozi wa timu na kocha Habib kusitisha mkataba. Tunamshukuru kocha Habib kwa kipindi chote alichofanya kazi na sisi.”
–
Kondo anaondoka Mtibwa ikiwa nafasi ya 15 baada ya kukusanya pointi 2 kwenye mechi 5 wamepoteza 3 na kupata sare 2.
Home Mtibwa yaachana na Habib Kondo
Comments are closed.