Mtibwa yaachana na Mayanga

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umemfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga kutokana na mwenendo mbaya wa timu kwenye michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Azam Sports Federetion (ASFC).

Akizungumza na HabariLEO, Afisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru ameeleza kuwa uongozi wao umefikia maamuzi hayo kwa nia njema ya kuinusuru timu hiyo isishuke daraja.

“Nimaamuzi magumu kutokana na kocha Mayanga kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa timu hii lakini nadhani upepo mbaya umempitia na kudumu kwa muda mrefu kwake kiasi cha kuiweka timu katika hatari ndiomaana uongozi umeamua kumpumzisha,” amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar nimiongoni mwa timu ambazo huenda zikashuka daraja au kucheza michezo miwili ya mtoano ‘Play Off’  endapo haitashinda mechi zake tatu za mwisho, timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 29 katika michezo 27.

Habari Zifananazo

Back to top button