Mtoto miaka 9 amuakoa mtoto mwenzake ajali ya moto

MTOTO wa miaka tisa amedaiwa kumuokoa mtoto mwenzake wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa ndani baada ya nyumba yao kuanza kuteketea kwa moto mtaa wa Mhongolo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Imedaiwa nyumba hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Mjane Asha Maziku ambapo alieleza kuwaacha wijukuu zake nyumbani huku akienda kwenye shughuli zingine za kifamilia.

Akiongea na mwandishi wa gazeti leo nyumbani kwake Maziku amesema anafikiri chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme sababu alielezwa na mashuhuda kuwa Moto ulianzia kuwaka juu ya nyumba na awali shoti ya umeme ilikwisha wahi tokea kwenye nyumba hiyo.

“Nina ishi na wijukuu zangu wanne wawili wanasoma ambapo ndani kulikuwa na watoto hao wadogo Moto ulivyoanza walibebana kutoka nje hakuna aliyefariki bali Mali zangu zote zimeteketea ndani”amesema.

Maziku amesema kuna watu amesikia walisema ni jiko la gesi limesababisha lakini siyo kweli kwani mtungi wa gesi uliisha ni kipindi cha miezi sita sasa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x