Mtoto umri wa miaka mitatu auawa

MTOTO mwenye umri wa miaka mitatu (jina limehifadhiwa) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika kijiji na kata ya Lichingu wilayani Newala mkoani Mtwara.

Akizungumza leo mkoani Mtwara, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Mtaki Kurwijila – ACP amesema tukio hilo limetoa Novemba 8, 2023 majira ya saa 11 jioni ambapo mtoto huyo ameuawa na mtu aliyejulikana na kwa jina la Osward Dadi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya (35) hadi (40) mkazi wa kijiji hicho.

Mtoto huyo alikuwa akicheza na wenzake nyumba jirani na mtuhumiwa anapoishi, baada ya muda mtuhumiwa alimwita ndani mtoto huyo wakati watoto wenzake wakiendelea kucheza nje ambapo aliingia ndani humo kisha kufanikiwa kumkata kwenye koromeo na kusababisha mtoto huyo kutoka damu nyingi na kupelekea kifo hicho.

‘’Aliweza kusababisha mauaji hayo kwa kutumia kitu chenye ncha kali na hatimaye akachukua mwili akauhifadhi katika mfuko wa shangazi kaja yaan jina maarufu shangazi kaja, baada ya muda mama wa marehemu aliweza kumtafuta mtoto wake ndipo ilibainika kwamba mtoto huyo alikuwa ameingia pale ndani katika nyumba ya mtuhumiwa’’amesema Kurwijila

Ameongeza kuwa, ‘’Baada ya hapo ndipo iliweza kubainika kuwa mtuhumiwa alisababisha kifo cha yule mtoto kwahiyo tunamshikilia mtuhumiwa huyo kwa tuhuma hizo za mauaji na hatimaye kufikishwa katika vyombo vya sheria’’amesema

Kaimu kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wote mkoani humo kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kwa kupinga matukio yote ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kama ilivyotokea kwa mtoto huyo mdogo mbaye hana hatia yoyote.

Aidha mtuhumiwa huyo baada ya kutokea tukio alishambuliwa na wananchi wenye hasira kali lakini jeshi hilo la polisi lilifanikiwa kumuokoa akiwa amepata majeraha mengi katika mwili wake hivyo alifikishwa katika hospitali ya wilaya ya Newala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, mtuhumiwa baada ya kupata nafuu anatarijiwa kufanyiwa mahojiano na jeshi hilo ili waweze kujua chanzo na sababu za msingi za yeye kuweza kufanya mauaji ya mtoto huyo na katika uchunguzi wa awali na inaonyesha kuwa mtuhumiwa hana historia ya ugonjwa wa akili ni mzima.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button