Mtoto wa Ali Choki aacha ukurugenzi Extra Bongo sababu ya Bongo Fleva

DAR ES SALAAM: MTOTO wa mwanamuziki mashuhuri nchini Ali Choki, Choki Junior amejiengua katika bendi ya Extra Bongo inayomilikiwa na baba yake ili aweze kutumikia kazi yake ya utayarishaji wa wa muziki wa Bongo Fleva.

Choki Jr, amesema ameshindwa kuendelea kutumikia sehemu mbili kwa sababu sehemu zote zinahitaji muda wa kutosha na tayari alishaingia mikataba na baadhi ya wasanii wa bongo fleva ili wafanye kazi zao.

“Mimi nina fani nyingi ikiwemo utayarishaji wa muziki, niliingia mikataba na watu wengi kwa ajili ya kuwatayarishia nyimbo zao lakini pia kuna makampuni nayafanyia kazi hivyo nakosa muda sababu majukumu ni mengi, nimeamua muda mwingi niuelekeze kwenye mikataba yangu niliyoingia na wasanii pamoja na makampuni mbalimbali,” ameeleza.

Advertisement

Choki Jr, amesema kwa kuwa yeye ni mmoja wa wakurugenzi katika bendi ya Extra Bongo hivyo kujitenga kwake hakutoathiri bendi hiyo inayoongozwa na Ali Choki pamoja na Katapila.

Choki Junior amesema baada ya sikukuu ya Iddi ataachia wimbo wake mpya akiwa nje ya Extra Bongo.