Mtoto wa mfua vyuma ‘Messi’ atimiza ndoto zake

Ni mtoto wa Meneja wa kiwanda cha chuma alifanya kazi katika warsha ya utengenezaji wa sumaku huko Rosario, Argentina. Jorge Messi baba mzazi wa Lionel Messi alimzaa mtoto huyu Juni 24, 1987 na kuwa mtoto wa tatu kati ya wanne.

Baba yake ana asili ya Kiitaliano na Kihispania, mjukuu wa wahamiaji kutoka eneo la kaskazini-kati la Adriatic Marche la Italia, na kwa upande wa mama yake, ana asili ya Kiitaliano.

Anaitwa Lionel Messi mchezaji anayedhaniwa kuwa bora wa muda wote wa Taifa la Argentina licha ya wengine kuhisi kuwa ni Maradona ndiye anastahili nafasi hiyo. Baada ya takribani miaka 20 Messi anashinda ubingwa wa Kombe la Dunia.

Baada ya kufanya makubwa ndani ya miaka hiyo kwa kuchukua Ballons d’Or saba, lakini kitu pekee ambacho hakuwahi kufanya ni kuchukua Kombe la Dunia. Furaha ya Messi unaweza usiielezee leo.

Mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, Messi alishindwa kutamba mbele ya vijana wenye damu ya Adolf Hitler timu ya Taifa ya Ujerumani kwa kupoteza bao 1-0 lililofungwa na Mario Gotze na ndoto za Messi kuishia hapo.

Mwaka 2018, Messi akiwa na shauku za kutwaa ubingwa wa dunia, zilishindikana baada ya kutolewa na Ufaransa katika 16 bora. Leo Argentina imelipa kisasi.

Messi amefanikisha ndoto zake za muda mrefu kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia baada ya kushindi wa mabao 4-2 kwa penalty dhidi ya Ufaransa, baada ya dakika 90 kuisha sare ya mabao 2-2. mabao yamefungwa na Messi mawili na Di Maria na Mbappe matatu.

Messi anamaliza michuano hiyo akiwa mfungaji bora akiwa na mabao saba, na pasi za mabao nne, lakini amefikisha mabao 13 ya Kombe la Dunia. lakini ni bao lake la 793 katika maisha yake ya soka.

Sio hivyo tu, akiwa na umri wa miaka 35 Messi anakuwa mchezaji wa kwanza, kufunga kila raundi ya Kombe la Dunia, kwamaana amefunga kwenye makundi, 16, robo fainali, nusu hadi fainali anaitwa Leonel Messi, La Pulga (Kiroboto).

Messi sasa anastaafu rasmi timu ya Taifa, Messi utakumbukwa mpira utakukosa, mashabiki watakulilia. hakuna Messi asichokifanya kwenye mpira wa miguu. Kwaheri Messi.l

Habari Zifananazo

Back to top button