Mtoto wa Museven autaka urais

MTOTO wa Rais wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba amesema amechoka kusubiri kuwa rais Uganda na ni muda sasa wa kuanza harakati za kushika nafasi hiyo.

Akizungumza jana, Muhoozi alisema hivi karibuni atatoa msimamo wake kuhusu suala hilo.

“Mawaziri Wakuu wa Uingereza na Finland wana umri wa miaka 42 na 37, wakati nakaribia miaka 50 na bado anasubiri kuwa mkuu wa nchi.

”?amehoji Muhoozi.

Matamshi yake yanakuja kinyume na matamshi aliyotoa siku za nyuma ambapo alisema kuwa lazima awe rais baada ya baba yake, Yoweri Museven kutoka madarakani.

Miezi michache iliyopita, Muhoozi alisema kuwa njia pekee ya kumfanya mama yake ajivunie ni kuwa kiongozi wa Uganda.

“Njia pekee ninayoweza kumlipa mama yangu ni kwa kuwa Rais wa Uganda, nina uhakiia nitafanya hivyo”.

alisema Muhozi.

Habari Zifananazo

Back to top button