MTOTO wa Ronaldinho, joao Mendes amesaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Barcelona, kwa mujibu wa mwandishi wa michezo Fabrizio Romano.
Mendez 17, amesaini mkataba huo kwa mara ya kwanza katika kuanza maisha yake ya soka akisimamiwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo.
“Nimefurahi sana na nina furaha kwa nafasi hii kubwa.”Mendes amesema
Ronaldinho pia aliwahi kucheza Barcelona kuanzia 2003 hadi 2008 alipotimikia AC Milan ya Italia.