Mtoto wa siku mbili atupwa chooni

MTOTO anayekadiriwa kuwa na umri wa siku mbili amenusurika kifo baada ya kutupwa chooni na mama yake mzazi mara baada ya kujifungua huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugumu wa maisha ikiwemo kukataliwa na baba wa mtoto.

Akizungumzia tukio hilo ofisa ustawi wa Jamii Halmashauri ya Nsimbo Teresia Mwendapole amesema mtoto huyo baada ya kuokolewa alipelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi ambapo anaendelea kupatiwa matibabu.

“Mtoto huyo alitupwa na mama huyo chooni kutokana na changamoto ya kukataliwa na wanaume na habari nyingine nyingine,tulimpokea akalazwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa na sasa anaendelea vizuri kwa usimamizi wa maofisa ustawi”

Nae Diwani viti maalum Kata ya Uruwila Fortunata Gerald amesema baada ya kumuangalia mtoto huyo alionekana kitovu kilikuwa kimeshaanza kunyauka huku akimkadiria kuwa ana siku zaidi ya mbili.

“Mimi kama mzazi ambaye nimeshapitia mambo ya uzazi nilimuhisi yule mtoto kama ana siku tatu mule ndani, baada ya kuuliza wakaniambia kwamba yule mtoto wamemkuta ameanguka amelala kwa kifudifudi amefumba mdomo na mikono akiwa amepiga magoti na kondo likiwa pembeni limekatwa”

Nao baadhi ya majirani wa kijiji hicho wamelaani tukio hilo huku wakiliomba Jeshi la Polisi kumchukulia hatua aliyehusika na tukio hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya watoto Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi Dokta Maria Matei amethibitisha kumpokea mtoto huyo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake huku akieleza hali ya mtoto huyo kuwa anaendelea salama.

“Tulimpokea akiwa na majeraha sehemu za uso,miguu na mikononi,tulimpatia matibabu ambayo kwa sasa anaendelea vizuri yuko chini ya uangalizi wa matibabu lakini akiwa anaendelea na matibabu na afya yake imeimarika”

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame amekiri kutokea kwa tukio hilo na tayari upelelezi umekamilika ikiwa ni pamoja na jalada lake kufikishwa kwa mwendesha mashtaka wa serikali wakati mtuhumiwa akiwa nje kwa dhaman

Habari Zifananazo

Back to top button