MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amepokea na kuzindua vifaa vya kisasa vya uchimbaji wa visima vya maji na mabwawa, yakiwemo magari mawili.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh bilioni 45 vimekabidhiwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mtwara.
Akiongea katika hafla ya kupokea vifaa hivyo Wilaya ya Nanyumbu mkoani humo, Kanali Abbas amesema vifaa hivyo vitatumika katika mkoa, wilaya na halmashauri kwa ajili ya kuchimba visima vya maji na mabwawa.
Amesisitiza umuhimu wa kutunza vifaa hivyo, ili viweze kusaidia kwa muda mrefu kutatua changamoto ya maji Mtwara.