MKUU wa Wilaya ya Mtwara Dustan Kyoby, amesema mwitikio wa wananchi ni mzuri katika Sensa ya Watu na Makazi 2022.
Kyobya amesema hayo mapema leo, mara baada ya kuhesabiwa yeye pamoja na mke wake katika Makazi yao eneo la Shangani mjini Mtwara.
Amesema sense Wilaya ya Mtwara, Halmashauri zote tatu lilianza vizuri maeneo ya hotelini, kiwanda cha Saruji Cha Dangote, pamoja na hospitalini.
“Asubuhi ya leo zoezi limeendelea, ambapo katika maeneo mbalimbali watu wanahesabiwa, muitikio ni mzuri zaidi na naomba wananchi waendelee kujitokeza,” amesema.