Mtwara Mjini wasifu utendaji wa serikali

WANANCHI wa Jimbo la Mtwara Mjini wameipongeza serikali kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jimboni humo, mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga amesema maeneo mengi aliyotembelea wananchi wamekuwa wakitoa salamu za pongezi kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kutokana na uongozi uliotukuka.

‘’Kwa niaba ya wapiga kura wa jimbo la mtwara Mjini kabla hatujaingia kwenye mwaka mpya 2024, maeneo mengi niliyopita wananchi walikuwa wananieleza tupelekee salamu zetu za kumpongeza Rais wetu Dk Samia.’’amesema Mtenga.

Serikali imetatatua changamoto mbalimbali ndani ya jimbo hilo ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, migogoro ya ardhi ikiwemo wa uwanja wa ndege ambapo yote hayo ni kupitia jitihada zinazofanywa na mbunge huyo katika ufatiliaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo jimboni humo.

Aidha, amepongeza utendaji kazi unaofanywa na Mkurungenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo, Mwalimu Nyange kutokana ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu aripoti katika manispaa hiyo amekuwa na usimamizi nzuri wa ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato kwenye manispaa hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mtwara Salum Naida amesema: ‘’Kamati ya siasa wilaya tumeona ipo haja ya kukutana na waandishi wa habari ili apate kueleza namna anavyotekeleza Ilani lakini pia Rais Samia anavyotuletea pesa nyingi katika miradi mbalimbali ya kimkakati katika mkoa wetu wa mtwara na ndani ya jimbo.”

Habari Zifananazo

Back to top button