Mtwara wafikia sensa asilimia 91

Mtwara

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mkoani Mtwara, imefikia asilimia 91.

Amewaambia waandishi wa Habari ofisini kwake mapema leo kuwa mpaka kufikia muda wa kufungu  shughuli ya sense leo usiku, mkoa huo utakuwa umefikia asilimia 100.

“Mpaka jana saa mbili usiku tulikuwa tuna asilimia 91 na leo makarani wapo tena kwenye maeneo ya kuhesabia kuhakikisha mpaka tunafunga zoezi tuwe tumekamilisha asilimia 100,” amesema.

Advertisement

Amesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa, huku akitaja changamoto kidogo kuwa ni maeneo ya mijini, ambapo makarani wakifika kwenye baadhi ya maeneo ya kuhesabia hawakuti wananchi.

“Changamoto tumeipata kwenye maeneo yote ya mjini kwa maana ya hapa mkoani na wilayani kutokana na shughuli za kimaendeleo za wananchi, kwa hiyo ukienda kuwahesabu unakuta wameshaondoka kwenda Kwenye shughuli zao za kujitafutia,” amesema.

Hata hivyo amesema mkoa umebuni utaratibu wa kuweka makarani ambao wanakwenda baada ya saa za kazi kwa ajili ya kuhesabu wananchi, ambao walienda kwenye shughuli zao.