Mudathir aipeleka Yanga kileleni
#DAR ES SALAAM: BAO pekee lililofungwa na Mudathir Yahya katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC, limeifanya Yanga kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi tisa.
–
Mudathir amefunga bao hilo katika dakika ya 88, baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukuwa nafasi ya Pacome Zouzoua.
–
Kabla ya mchezo huo, Yanga ilikuwa nafasi ya pili, wakiwa na pointi sita, wakati Mashujaa walikuwa nafasi ya kwanza na baada ya ushindi wa Yanga, timu hiyo imerudi hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi saba.
–
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, hakuna timu iliyokuwa imeonja utamu wa lango la mwenzake.
–
Kesho kutakuwa na michezo miwili ya ligi hiyo, Simba dhidi ya Coastal Union mchezo utapigwa uwanja wa Uhuru saa 10:00 Alasiri.
–
Azam itakuwa Chamazi Complex dhidi ya Singida Big Stars mchezo utachezwa saa 1 usiku.’