Mudryk ameanza hivyo

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Mykhailo Mudryk amefunga bao la kwanza jana akiwa na Chelsea.

Mudryk alisajiliwa Chelsea Januari 15, 2023 kwa ada ya uhamisho wa £88.

5m akitokea FC Shakhtar Donetsk.

Katika mchezo wa jana wa EPL dhidi ya Fulham ulioisha kwa Chelsea kushinda mabao 2-0, Mudryk alifungua akaunti ya mabao dakika ya 18 akipokea pasi kutoka kwa Levi Colwill.

Baada ya ushindi huo, ‘The Blues’ imepanda hadi nafasi ya 11, ikiwa na pointi 8, katika michezo saba waliyocheza.

Ratiba inaonesha wikiendi hii, Chelsea itakabiliana na Burnley, kisha Arsenal, Brentford, Spurs, Man City, Newcastle, Brighton, Man United.

Habari Zifananazo

Back to top button