Mudryk kutimkia Arsenal?

LONDON, England: Wababe wa soka kutoka London kaskazini Arsenal wanahusishwa na kumnunua winga wa klabu ya Chelsea ya jijini humo Mykhailo Mudryk katika majira ya joto.
 
Mudryk alisajiliwa Chelsea kutoka Shakhtar Donetsk ya Ukraine Januari 2022 kwa ada ya pauni milioni 89 ikijumuisha nyongeza lakini hadi sasa hajaonesha makali ya thamani hiyo.
 
Licha ya kuanza vibaya maisha yake ya soka ndani ya klabu ya Chelsea, Arsenal inaripotiwa kuwa na nia ya kumhamishia London Kaskazini, kwa mujibu wa jarida la Spain la Fichajes.net
 
Ripoti hiyo imebainisha kuwa Chelsea itasikiliza ofa kwa winga huyo mwenye umri wa miaka 23, lengo kuu likiwa ni uhamisho wa mkopo ili kukuza kiwango chake. Juventus pia wanahusishwa kuitaka saini yake

Habari Zifananazo

Back to top button