Mufti ataka Waislamu kuchangia mafanikio ya Uislamu

Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi

SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi amewataka Waislamu kujenga tabia ya kujitolea fedha na mali zao kwa ajili ya kuendeleza mafanikio ya Uislamu.

Mufti ameyasema hayo Jumatano wakati  akiwaongoza viongozi wa dini ya Kiislamu wa wilaya na kata wakiwemo mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kwenye dua ya kuombea Msikiti wa Mucaddam uliopo Kata ya Chang’ombe jijini Dodoma.

Aliwataka waumini wa Kiislamu hapa nchini kuwa na tabia ya kupenda mafanikio ndani ya Uislamu ikiwemo kujenga majengo mbalimbali kama vile misikiti na madrasa.

Advertisement

Hata hivyo, amewapongeza waumini wa msikiti huo kwa kujitolea kwa mali na fedha na kuweza kufanikisha kujenga msikiti huo wa ghorofa mbili.

Alisema juhudi zilizofanywa ni mfano mzuri wa kuigwa kwa waumini wengine ili kwenye maeneo yao wanayoishi waweze kujenga majengo ya misikiti kwa ajili ya maendeleo.

Awali akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa msikiti huo wa Muccadam wa Chang’ombe jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza la Bakwata Wilaya ya Dodoma, Bashir Hussen alisema ujenzi huo ulianza Septemba 2021 kwa juhudi za waumini wa msikiti huo na baadhi ya marafiki ambao umetoa michango yao ya mali na fedha.

“Msikiti wa hapo mwanzo ulikuwa na hali mbaya sana lakini kutokana na kauli ya Bakwata ile inayosema Jitambue, Badilika na acha Mazoea tumeifanyia kazi na sasa tumeweza kujenga msikiti huu wa ghorofa tatu kwa nguvu zetu,” alisema.

 

 

/* */