MUHAS waanza kutoka wataalam wa moyo

CHUO cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kimeanza kutoa wataalamu  wa upasuaji kifua na moyo mafunzo yaliyotolewa nchini.

Mafunzo hayo yametokana na ushirikiano baina ya MUHAS na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayesimamia Taaluma, Profesa Emmanuel Balandya amesema kuwa hatua hiyo ni kuhakikisha kwamba wanapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu mbalimbali.

Amesema chuo hicho kinaendelea kuzalisha wataalamu waliobobea katika magonjwa mbalimbali.

Ameeleza kuwa kati ya programu 84 zinazotolewa chuoni hapo, 20 ni za uzamivu  na ubobezi katika magonjwa  ya moyo, figo, mfumo wa upumuaji, tiba mionzi, uvumbuzi wa magonjwa ya fahamu kwa njia ya mionzi, matumizi ya picha kwa uvumbuzi wa mago jwa ya uzazi kwa wanawake na utoaji wa damu.

Pia yapo magonjwa ya mfumo wa fahamu, upasuaji wa mifumo ya fahamu, upasuaji wa moyo, usingizi katika upasuaji wa moyo, upasuaji rekebishi, mgonjwa ya njia ya mkojo, wagonjwa mahututi na magonjwa ya watoto wachanga.

“Programu nyingine ni za saratani za damu kwa watoto, magonjwa ya mfumo wa chakula na pua,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x