MOI kuwapigia simu wagonjwa kujua hali zao

TAASISI ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), itaanza utaratibu wa kuwapigia wagonjwa simu au kutuma ujumbe mfupiwa maandishi ili kuwajulia hali, kupata maoni na kuwapa ushauri .

Utaratibu huo utawezesha wagonjwa kuwa na nafasi ya kutoa maoni au kueleza changamoto zao wakiwa nyumbani kabla ya kurudi tena katika kliniki za ufatiliaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Prof.

Abel Makubi, amesema hayo leo wakati wa kikao na watoa huduma kwa wateja pamoja na walinzi, ili kukumbushana misingi bora ya utoaji huduma kwa wateja na kupunguza mahangaiko na malalamiko kwa wateja.

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao baina ya Prof. Makubi na makundi mbalimbali ya watumishi wa MOI, lengo likiwa ni kutatua changamoto ili kuleta mabadiliko na matokeo chanya katika utoaji huduma kwa wateja.

“Kupitia kikao hiki ni vyema kukumbushana namna sahihi ya upokeaji wa wagonjwa, ikiwemo utoaji wa lugha za staha na za kiungwana, ili kumfanya mgonjwa afurahie huduma pindi afikapo katika Taasisi yetu ya MOI,” amesema Prof. Makubi.

Habari Zifananazo

Back to top button