Muhimbili-Upanga sasa kuweka puto tumboni

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili MNH, imezidi kujiimarisha katika kuboresha huduma zake ikiwemo uwekaji wa puto tumboni kwa watu wanaohitaji kupunguza uzito wa mwili.

Huduma hiyo ambayo imeanza kutolewa mwishoni mwa mwaka 2022 tayari imehudumia watu 151 ambapo 150 wamehudumiwa MNH-Mloganzila na mmoja katika MNH-Upanga huduma ambayo imeanza kutolewa mwishoni mwa wiki hii.

Hayo yamezungumzwa na Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji Mfumo wa Chakula, Ini na Mbobezi wa Upasuaji Kutumia Matundu Madogo MNH, Dk Kitembo Kibwana na kusisitiza kuwa lengo ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo.

Advertisement

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *