MKAZI wa Kiluvya Madukani wilayani Kisarawe, Primrose Matsambire (39) amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alisema Januari 11 mwaka huu, Matsambire alikuwa akitokwa na damu mdomoni akiwa nyumbani kwake.
Alisema jana kuwa Matsambire alifariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
“Mtu aliyegundua marehemu kutokwa damu mdomoni ni msichana wa kazi na ndipo alipoomba msaada kwa majirani ambao walimpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu,” alisema.
Kamanda Lutumo alisema wakati tukio hilo linatokea mume wa marehemu, Michael Chipindula hakuwepo nyumbani na anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano na uchunguzi kuhusu kifo cha mkewe.
“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi huku chanzo cha kifo hicho kikiendelea kuchunguzwa,” alisema
Comments are closed.