Mume wa Kamala atembelea Kikwete youth park

MWENZA wa Makamu wa Rais wa Marekani, Douglas Emhoff leo Machi 30, 2023 ametembelea kituo cha kukuza vipaji vya michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Katika zira hiyo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk Pindi Chana ameshiriki pamoja na Emhoff na kupata fursa ya kufanya ziara fupi kuona jinsi kituo hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuzungumza na vijana wanaofundishwa mpira wa miguu na kikapu katika Kituo hicho.

Emhoff amewasihi vijana hao wajifunze kwa ari na bidii ili waje kuwa nyota wazuri na wakubwa duniani.

Waziri Balozi Dk Pindi Chana amemshukuru mwenza huyo kwa ziara yake katika Kituo hicho ambapo amesema ni miongoni mwa vituo vinavyolea vipaji ambavyo vinatarajiwa kuisaidia nchi katika Sekta ya michezo.

Balozi Dk Pindi Chana amesema kuwa ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan imefungua milango kwa wadau ndani na nje ya nchi kuona fursa zilizopo nchini katika Sekta za Michezo, Utamaduni na Sanaa na kuzitumia katika kuleta maendeleo kwa mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

 

Habari Zifananazo

Back to top button