Museven atuma vikosi wanafunzi waliouawa

Ugandan security forces stand guard as locals gather at the cordoned scene outside the Mpondwe Lhubirira Secondary School, after militants linked to rebel group Allied Democratic Forces (ADF) killed and abducted multiple people, in Mpondwe, western Uganda, June 17, 2023. REUTERS/Stringer

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ametuma vikosi vya kijeshi Mashariki mwa taifa hilo, ambako imeripotiwa kundi linalodhaniwa kuwa ni Islamic State (IS) limeua wanafunzi 37 wa shule moja ya sekondari jana. Mtandao wa Habari Reuters umeripoti.

Wanachama waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) waliwaua wanafunzi hao Ijumaa jioni katika Shule ya Sekondari ya Lhubirira iliyoko Mpondwe karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi na polisi walisema washambuliaji hao pia waliwateka nyara wanafunzi sita na kutoroka kuelekea Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga kuvuka mpaka. Hatima yao haijulikani.

Advertisement

Museveni alisema wanajeshi zaidi walijiunga na msako huo katika eneo hilo, ambalo ni pamoja na Mlima Rwenzori, ambapo ADF ilianzisha uasi wao dhidi ya Museveni katika miaka ya 1990. Kwa mujibuwa Reuters.

“Sasa tunatuma wanajeshi zaidi katika eneo la kusini mwa Mlima Rwenzori,” alisema katika taarifa.

“Kitendo chao, hatua ya kukata tamaa, ya woga, ya kigaidi, kwa hiyo, haitawaokoa. Tunaleta vikosi vipya upande wa Uganda tunapoendelea na uwindaji upande wa Congo.”

Siku ya Jumamosi, televisheni ya kibinafsi ya NTV Uganda ilisema idadi ya waliofariki ilifikia 41, huku gazeti la serikali la New Vision lilisema walikuwa 42.

New Vision ilisema 39 kati ya waliofariki ni wanafunzi, na wengine waliuawa wakati washambuliaji walipotega bomu na kukimbia.

Shambulio hilo lilizua shutuma nyingi za kimataifa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki. Raia wa Uganda walishangazwa na shambulio hilo.

“Wazazi kote nchini, tafadhali msiwe na hofu, watoto wetu wako salama, na watabaki salama. Ni watu waovu na wanajaribu kuwadhuru watoto wetu, lakini hawataweza,” Janet Museveni, Mke wa Rais na Waziri wa Elimu alisema.