Musk afunguliwa mashtaka malezi ya watoto

MKURUGENZI wa kampuni ya maswala ya anga Space X, Elon Musk amefunguliwa mashtaka na mzazi mwenzake, mwimbaji Claire Boucher (35) kuhusu haki za malezi kwa watoto wao watatu.

Boucher anayejulikana kwa jina la ‘Grimes’ awali alimshutumu Musk kwa kumzuia kumuona mwanaye wa kiume katika ujumbe ambao umefutwa kwenye mitandao ya kijamii.

Musk mwenye umri wa miaka 52 ana watoto 11 ambao amewapata kwa wanawake watatu tofauti.

Maelezo ya ombi hilo, lililowasilishwa kwa Mahakama ya Juu ya San Francisco hata hivyo sio Grimes wala Musk aliyefikiwa kutoa maoni yake juu ya suala hilo.

Grimes na Musk wana watoto watatu anayejulikana kama X, ambaye alizaliwa Mei 2020, na binti anayeitwa Exa Dark Sideræl – anayejulikana kama Y – ambaye alizaliwa kwa Disemba 2021.

Mtoto wa tatu, mvulana anayeitwa Techno Mechanicus, au Tau, alizaliwa Juni mwaka jana.

Katika chapisho lililofutwa tangu mwezi uliopita, Grimes alimwambia Musk “niruhusu nionane na mwanangu au nimjibu wakili wangu”.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button